RAIS WA MAREKANI BARAKI OBAMA AMEKIRI ALIKOSEA KUTATUA MZOZOZ LIBYA. - Rhevan Media

RAIS WA MAREKANI BARAKI OBAMA AMEKIRI ALIKOSEA KUTATUA MZOZOZ LIBYA.

ObamaImage copyright
Image captionRais Obama amekiri kwamba Marekani ilikosea katika kutatua mzozo Libya
Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.
Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.
Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.
Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.
GaddafiImage copyrightGetty
Image captionEneo la Sirte, alikozaliwa Gaddafi, lilishambuliwa sana na majeshi ya muungano
Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.
Gaddafi
Image captionMuammar Gaddafi aliuawa na wapiganaji
Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.
Previous
Next Post »