RAIS MAGUFULI AMWAGIWA UFAGIO KIGOMA. - Rhevan Media

RAIS MAGUFULI AMWAGIWA UFAGIO KIGOMA.



Mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM) Mkoa wa Kigoma peter Msanjilla akiongea na mwandishi wa habari hii ofisini kwake(hayupo pichani) baada ya kikao cha kamati ya  utekelezaji umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kigoma

Na Editha Karlo wa blog ya jamii Kigoma. 

UMOJA wa vijana wa chama cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Kigoma wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kazi yake nzuri anayofanya ya kuwatumikia wananchi tangu alipoingia madarakani. 

Mwenyekiti wa umoja huo wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Peter Msanjilla, alimwambia mwandishi wa blog hii ofisini kuwa kamati ya utekelezaji ya vijana Mkoa wametoa pongezi hizo katika kikao kilichofanyika leo (jana) kwenye ofisi za CCM mkoa. 

Alisema kuwa wameamua kumpongeza Rais kwa sababu ya kasi yake anayofanya ya kudhibiti uchumi na kutaka nchi ijiendeshe kwa kutumia fedha za ndani. Msanjilla alisema kuwa pia katika kikao hicho wamemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya Rais kwa kusimamia vyanzo vya mapato vilivyopo katika Mkoa akishirikiana na mamlaka ya mapato nchini(TRA). 

"Hapa Mkoani kwetu kuna mahotel mengi tu na sheli za mafuta nyingi, lakini huwa hawatumii mashine za EFD kutoa risiti wao wanaandika kwa mkono hii haikubaliki ni sawa na luhujumu uchumi wa nchi"alisema Msanjille.

Pia umoja huo umempongeza mwenyekiti wa wazazi Taifa Alhaji Bulembokwa kuadhimisha wiki ya wazazi katika jumuiya hiyo ambapo Kitaifa inafanyika Mkoani Morogoro. 

Previous
Next Post »