Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika kijiji cha Busongola tarafa ya Mishamo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.
Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi SSP Damas Nyanda amesema kuwa watu hao wamekamatwa wakiwa na bunduki aina ya SMG 5971 ya mwaka 1996 pamoja na magazine mbile na risasi 86 nyama ya mnyama pori kiboko katika nyumba ya Amos Maliyatabu.
Kamanda ameongeza kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema walifika katika eneo la tukio ambapo majambazi hao walikuwa wakijipanga kufanya ujambazi na walipowaona Polisi walianza kupiga risasi hewani na polisi wakajibu mapigo na kufanikiwa kumuua jambazi mmoja na wengine wanne wanashikiliwa na jeshi hilo.
Aidha Kamanda Nyanda amewataka wananchi kutoa taarifa kila wanapoona au kuhisi kuna hali isiyokuwa ya usalama katika maeneo yao ili jeshi hilo liweze kuwajibika kuimarisha usalama.
Sign up here with your email
