NAIBU WAZIRI WA NCHI : BAJETI TAMISEMI IKAHUDUMIE WANANCHI HUSUSANI KATIKA MAENEO YA VIJIJINI. - Rhevan Media

NAIBU WAZIRI WA NCHI : BAJETI TAMISEMI IKAHUDUMIE WANANCHI HUSUSANI KATIKA MAENEO YA VIJIJINI.

Serikali imejikita kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma na kuhakikisha watanzania wanaboreshewa huduma mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya, na huduma za mama na mtoto.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo amesema bajeti pendekezwa iliyopitishwa na serikali ya shilingi trilioni 6 kwa wizara yake ipelekwe ikahudumie wananchi hususan katika maeneo ya vijini.
Mhe. Jafo ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano uliowakutanisha viongozi wa serikali kutoka mikoa mbalimbali na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na TAMISEMI mkutano wenye lengo la kujadili bajeti iliyopendekezwa.
Aidha, Mhe. Jafo ameongeza kuwa serikali imejikita kusimamia matumizi sahihi ya fedha za umma na kuhakikisha watanzania wanaboreshewa huduma mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya, na huduma za mama na mtoto.
Akisoma mapendekezo ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na TAMISEMI Dkt. Pudenciana Kikwembe amesema tatizo waliloliona kwa baadhi ya vipengele vya bajeti hiyo ni pamoja na vipengele vya huduma ya hospitali kuwa na bajeti isiyojitosheleza na swala la maji hivyo serikali iangalie namna nzuri ambayo italenga wananchi katika kuleta maendeleo na kuangalia unafuu wa maisha.
Previous
Next Post »