MKUU WA MKOA WA MOROGORO AWAKAMATA WACHINA WAWILI NA KUWALAZA NDANI. - Rhevan Media

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AWAKAMATA WACHINA WAWILI NA KUWALAZA NDANI.



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe, (katikati) pamoja na ujumbe wake wakifanya ukaguzi wa kushitukiza katika mgodi wa Kiwanda cha Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd , katika mgodi wa Kiwanda hicho uliopo eneo la Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro, kiwanda hicho kinamilikiwa na wachina, uzalishaji wake ulizuiwa na Serikali kuu tangu mwaka 2010 hadi watakapokamilisha taratibu zote za kisheria zikiwemo na za kimazingira.
Mfanyakazi raia wa China, Wang Jun (33) ambaye ni mtunza stoo katika mgodi wa kutengeneza marumaru wa Kiwanda cha Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd ,kinachomilikiwa na Wachina akiwa chini ya ulinzi wa Polisi kufuatia ukaguzi wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Steven Kebwe, Aprili 13,2016 akifuatana na ujumbe wa serikali ya mkoa na wilaya ya Morogoro katika mgodi wa Kiwanda hicho uliopo Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Tarafa ya Mikese , ambapo walikutwa wakiendelea na uzalishaji licha kuzuiwa na Serikali kuu mwaka 2010 hadi watakapokuwa wamekamilisha taratibu zote za kisheria zikiwemo na za kimazingira.

Na John Nditi, Morogoro

RAIA  wawili wa China wametiwa nguvuni mkoani Morogoro kutokana na kuendelea kusimamia shughuli za uzalishaji wa marumaru katika mgodi wa mawe wa Kiwanda cha Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd ,kinachomilikiwa na Wachina licha ya kuzuiwa na Serikali kuu tangu mwaka 2010.

Mbali na kuendelea na uzalishaji katika kipindi chote hicho, kampuni hiyo imekuwa ikifanya udangayifu  kuwa marumaru  zinazouzwa katika maduka yake zinaingizwa kutoka  nchini China , wakati bidhaa hiyo ikitengenezwa  kutoka Morogoro.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe, aliamuru kukamatwa kwa raia hao  baada ya kufanya  ukaguzi wa kushitukiza   Aprili 13, 2016  akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa  pamoja na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro.


Previous
Next Post »