MKUU WA MKOA MAKONDA UCHAFU WA MSHINDA. - Rhevan Media

MKUU WA MKOA MAKONDA UCHAFU WA MSHINDA.


Ukosefu wa majisafi na salama, vyoo bora pamoja na mila potofu zimetajwa kuongeza Changamoto ya kupambana na kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania ambapo hadi sasa ugonjwa huoumesababisha vifo vya watu 326.
Akitoa tamko kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Waziri wa afya, maendeleo ya jamii wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema licha ya vifo hivyo kasi ya ugonjwa huo imepungua.
Mhe. Ummy Mwalimu amesema mikoa 10 bado imeripotiwa kuwa na ugonjwa huo ambapo Mkoa unaoongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ni mkoa wa Mara wenye wagonjwa 128, ukifuatiwa na Kilimanjaro wagonjwa 89, Morogoro wagonjwa 41 pamoja na Dar es salaam wenye wagonjwa 31.
Waziri ameitaka Mikoa ambayo haina ugonjwa wa kipindupindu kuhakikisha anatunza mazingira na kukumbusha utaratibu wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi wananchi washirikiane katika kutunza mazingira.
Aidha Waziri amesema katika kipindi hichi cha mvua jamii imetakiwa kutumia majisafi na salama yaliyotakaswa kwa dawa ya waterguard au kuchemsha maji ili kuepuka kupata maambukizi ya kipindupindu.
Previous
Next Post »