MKUTANO WA DHARURA WAITISHWA SUDAN YA KUSINI. - Rhevan Media

MKUTANO WA DHARURA WAITISHWA SUDAN YA KUSINI.

Image copyright
Image captionkuunganisha taifa
Kamati ya pamoja inayosimamia mpango wa Amani nchini Sudan Kusini imeitisha mkutano wa dharura kujadili switafahamu inayokumba kurejea kwa kiongozi wa waasi Riek Machar jijini Juba.
Mwenyekiti wa kamati Festus Mugae amesema mkataba wa amani uko hatarini kufuatia hali hiyo. Nayo wizara ya maswali ya kigeni ya Marekani pia imeeleza kusikitika kwake na Machar, huku ikidai Machar anachelea kufika Sudan kimakusudi.
Joto la kidiplomasia linazidi kupanda kufuatia uamuzi wa Riek Machar kutofika Juba kwa siku ya pili mfululizo.
Msemaji wa wizara ya maswali ya kigeni wa Marekani John Kirby amesema kuchelewa kwa Machar ni makusudi na inahatarisha maisha ya wananchi wa Sudan Kusini.
Aidha kamati ya kusimamia mkataba wa Amani nchini humo pia imeeleza masikitiko yake dhidi ya Machar, lakini vilevile ikaipa changamoto serikali ya Sudan Kusini kulegeza kamba ili kumwezesha Machar kurejea.
Image captionRiek Machar
Siku ya Jummanne kambi ya waasi ilisema Machar hangerejea kwa sababu serikali ilikataa kutoa kibali cha kumruhusu makamu wake kuingia anga za Sudan Kusini.
Lakini serikali ilijibu kuwa Machar alitaka kuingia nchini na idadi isiyokubalika ya wanajeshi na silaha nzito.
Msemaji wa Machar Mabior Garang alisema serikali inadanganya, na kuashiria kuwa Riek Machar atawasili Juba hii leo kusipokuwa na hitilafu.
Kurejea kwa Machar ni hatua muhimu ya kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa sahihi mwezi Agosti mwaka jana.
Iwapo atarejea, ataapishwa kama makamu wa rais , kisha kutakiwa kuunda serikali ya muungano na rais Salva Kiir.
Image captionSalva Kiir
Riek Machar aliiaga Sudan Kusini mnamo mwaka wa 2013 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza.
Tangu hapo maelfu ya watu wameuawa, huku zaidi ya watu milioni mbili wakipoteza makao.
Previous
Next Post »