Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu amemfuta machozi Mwanadada, Happiness Millen Magese ambaye ni shujaa wa kipekee kutoka Afrika dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Endometriosis.
Mama Samia amechukua hatua hiyo jioni ya 15 Aprili 2016 wakati wa hafla maalum ya kumkabidhi tuzo.
Katika kilio chake hicho, Millen kimemfanya Mama Samia kumfuta machozi na kumpa kitambaa, mwanamitindo huyo huku akimweleza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana naye kwani tatizo hilo si la Millen pekee bali ni kwa wanawake wengi hapa Tanzania.
Mama Samia alimwambia kuwa, tatizo alilonalo la kuziba kwa mirija ya uzazi lipata ufumbuzi na kutaka asilie kwani Serikali inania njema kwa watu wake hivyo wataendeleza juhudi Zaidi huku akifungua milango na mwanadada huyo.
Mama Samia akimfuta machozi Millen ambapo alimwelezea kuwa kwa sasa asiie tena kwani Serikali itahakikisha inapambana na ugonjwa huo ilikusaidia wanawake wengi hapa nchini.
Suluhu alisema kuwa hata yeye tatizo kama hilo lipo katika familia yake, lakini ana amini kwa ushirikiano wa mwanamitindo huyo tatizo hilo linapewa uzito. Alisema kuwa ni kitu kilichokuwa kikimuumiza sana kichwa, ana amini kupitia Millen hata binti yake atapata nafuu.
"Nimefurahi kukutana nawe na Serikali haitakuangusha tutakuunga mkono katika kuhakikisha gonjwa hili linapata ufumbuzi na kutoa elimu kwa kila mtanzania kulitambua"alisema.
Mama Samia akieleza namna walivyopokea tatizo hilo la Millen ambapo amemweleza kuwa Serikali itaendelea kupambana nalo tatizo hilo hivyo kumuakikishia Millen na taasisi yake kumuunga mkono.
Akizungumza kwa upande wake Magese alisema amekuwa akifanya semina mbalimbali kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuwaelimisha wanawake kuhusu endometriosis.
Alisema Machi 30, mwaka huu Taasisi ya Millen Magese ilikusanya vijana (hususani wa kike) wapatao mia tano kutoka shule za Mugabe, Manzese, Salma Kikwete na Turiani, kuwafundisha, kuwatahadharisha na kuwatanabahi kuhusu Afya, Uenendo, Maisha yao ya kila siku na Changamoto zilizo mbele yao na hususani ikilenga zaidi watoto wa kike ambao wao ndio wahanga wa ugonjwa wa Endometriosis.
Sign up here with your email