Ligi kuu ya England inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo kadhaa, Jumamosi Norwich itaikaribisha Sunderland.
Everton nao watakuwa wenyeji wa Southampton, Man Utd watakuwa wenyeji wa Aston Villa katika dimba la Old Traford huku Newcastle wakimenyana na Swansea City.
West Brom watawaalika Watford nao Chelsea watakuwa darajani Stamford dhidi ya Manchester City.
Jumapili vinara wa ligi Leicester City watakuwa nyumbani dhidi ya West Ham, Bournemouth watawaalika Liverpool na Arsenal itamenyana na Crystal Palace.
Jumamosi 16 Aprili, 2016 (Saa za Afrika Mashariki)
Norwich v Sunderland 14:45
Everton v Southampton 17:00
Man Utd v Aston Villa 17:00
Newcastle v Swansea 17:00
West Brom v Watford 17:00
Chelsea v Man City 19:30
Jumapili 17 Aprili, 2016
Bournemouth v Liverpool 15:30
Leicester v West Ham 15:30
Arsenal v Crystal Palace 18:00
Sign up here with your email