MAWAZIRI WAPYA WA SELIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR WAMEKABIDHIWA OFISI TAYARI KWA KUANZA MAJUKUMU YA KAZI. - Rhevan Media

MAWAZIRI WAPYA WA SELIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR WAMEKABIDHIWA OFISI TAYARI KWA KUANZA MAJUKUMU YA KAZI.




Mawaziri wapya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, wamekabidhiwa ofisi tayari kutekeleza majukumu yao.Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini alikabidhi ofisi kwa waziri mpya Issa Haji Ussi Gavu na kumtakia kila la heri katika utekelezaji wa majukumu hayo mapya ya kumsaidia rais katika utendaji wa kazi za kila siku.Dk Mwadini alisema majukumu aliyopewa Waziri Gavu ni makubwa ambayo yanaonesha imani aliyokuwa nayo rais dhidi yake na kwamba anao uwezo mkubwa wa kumsaidia Rais kusimamia na kuendesha ofisi hiyo.
Aidha aliwataka watendaji wa wizara hiyo, ikiwamo taasisi zake kutoa kila aina ya ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha wanafanikisha malengo ya Serikali ya kutoa huduma kwa wananchi walioichagua baada ya kumweka madarakani Dk Shein aliyeshinda uchaguzi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Naye aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili, Dk Sirra Ubwa Mamboya akikabidhi ofisi kwa waziri mpya Hamad, alisema malengo ya Serikali ya kuhakikisha Zanzibar inajitosheleza kwa kilimo yatafikiwa tu kama juhudi zitachukuliwa na wataalamu waliopo kufanya kazi kwa kuzingatia uzalendo zaidi.
Previous
Next Post »