DAVID KAFULILA KWA MARA NYINGINE TENA MAHAKAMNI KESI YAANZA UPYA. - Rhevan Media

DAVID KAFULILA KWA MARA NYINGINE TENA MAHAKAMNI KESI YAANZA UPYA.



Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora, Aprili 25, mwaka huu, inatarajiwa kuamua kuendelea au kutoendelea na kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini, iliyofunguliwa na mbunge za zamani wa bunge hilo, David Kafulila.Uamuzi huo unatokana na hoja iliyotolewa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata, kwamba kesi hiyo itupiliwe mbali kwa madai kwamba ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo vya upande wa mlalamikaji vinaonyesha kuwa hakuna kesi ya kujibu.
Jaji Ferdinand Wambali alikubali ombi hilo na kutaka upande wa wajibu maombi wa pili na wa tatu katika kesi hiyo, wawasilishe ombi hilo kwa maandishi ifikapo kesho na mlalamikaji kuwasilisha majibu ya maombi hayo Aprili 18 au 19, mwaka huu.
Hata hivyo, Jaji Wambali alizikumbusha pande zote kwamba kazi ya mahakama ni kusikiliza na kutoa uamuzi na si kuongeza migogoro.Baada ya Malata kuwasilisha ombi hilo, akishirikiana na wakili wa mlalamikiwa namba moja, Hasna Mwilima, ambaye ni mbunge wa sasa wa Kigoma Kusini, mawakili wa Kafulila wakiongozwa na Prof. Abdallah Safari, walipinga ombi hilo kwa madai kwamba upende wa mwanasheria mkuu wa serikali na mlalamikiwa wanaingilia uhuru wa mahakama.
Previous
Next Post »