Azerbaijan na majeshi yanayotaka kujitenga katika eneo la Nagorno – Karabakh yamekubaliana kusitisha mapigano kuanzia leo kufuatia siku kadhaa za mapigano makali katika jimbo hilo linaloleta mvutano tangu mwaka 1994.
Wizara ya ulinzi ya Azerbaijan imesema operesheni ya majeshi ya Azerbaijan na Karabakh zimesitishwa.
Msemaji wa wizara ya ulinzi katika jimbo lililojitangazia uhuru la Nagorno Karabakh amethibitisha usitishaji huo wa mapigano mapema leo.
Mapigano hayo yalizuka mwishoni mwa juma ambapo kila upande ukilalamikia upande mwingine kwa kuchochea na matumizi ya silaha nzito.
Sign up here with your email