Muammar Gaddafi alikuwa ni tofauti na viongozi wengine waliowahi kutajwa kuwa madikteta duniani, ana mengi ya kukumbukwa na kusifiwa kwayo. Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuongozi wamekuwa wakieleza kusikitishwa kwao na kutotambua aina ya demokrasia ambayo baadhi ya watu wa Libya wanaililia kwa sasa na iwapo itaboresha au kuharibu kabisa maisha yao.
Muammar Gaddafi alizaliwa Juni 7, 1942 katika mji wa Sirte, katika familia ya Mohamed Abdulsalama Abuminiar na mama Aisha Ben Niran. Alijiunga na Jeshi la Libya mwaka 1965.
Alipokuwa kijana
alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri na Gamal Abdel Nasser, alipokuwa
akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka
1956.
Gaddafi alipanga njama
ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi na aliwahi
kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya katika mji wa
Benghazi, na kupanga mapinduzi ya tarehe 1 Septemba mwaka wa 1969.
Gaddafi alianza kujenga
itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani
kibichi.
Alikitumia kitabu chake
kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na mfumo uliyo
tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.
Sign up here with your email

