ABIRIA ZAIDI YA 40 WANUSURIKA KIFO . - Rhevan Media

ABIRIA ZAIDI YA 40 WANUSURIKA KIFO .

Abiria wapatao 40 wamenusurika kifo kufuatia busi walilokuwa wakisafiria kutoka wilayani Bariadi mkoani Simiyu kwenda Ushirombo mkoani Shinyanga kuacha njia na kupinduka.
 
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 alifajili katika kijiji cha Kidurya nje kidogo ya mji wa Bariadi ambapo bus hilo mali ya kampuni ya Lucuman aina ya Scania lenye namba za usajili T302 AUU, lilipoacha njia na kupinduka.
 
Wakizungumza na ITV eneo la tukio baadhi ya majeruhi waliokuwa katika bus hilo walikuwa na haya ya kueleza.
 
Akithibitsha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu ,Nnesmo Lyanga anaelezea chanzo cha ajali hiyo.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hosptal ya mji wa Bariadi, Dr.Saidi Mlowasha amesema amepokea majeruhi watatu ambao wamefikishwa hosptalini hapo na kutibiwa.
Previous
Next Post »