KOCHA MPYA WA CHELSEA NAYE JIPU HUENDA AKUAFUNGIWA MIEZI SITA. - Rhevan Media

KOCHA MPYA WA CHELSEA NAYE JIPU HUENDA AKUAFUNGIWA MIEZI SITA.

conte-antonio-conte-antonio_3443206
Ni siku moja baada ya uongozi wa Chelsea ya Uingereza kutangaza kumpa mkataba wa miaka mitatu kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte ambaye atajiunga na klabu yao mwishoni mwa msimu. Leo April 5 Antonio Conte ameripotiwa kuwa, huenda akafungiwa miezi sita kujihusisha na soka.
Muendesha mashtaka Roberto Di Martino kutoka Italia anaripotiwa na Sky Sports kuwa April 5 2016 ameendeleza shauri la Conte kutuhumiwa kwa upangaji wa matokeo ya mechi ya ushindi wa Siena wa goli 1-0 dhidi ya Albinoleffe May 2011 na sare ya goli 2-2 dhidi yaNovara May 2011.


Antonio Conte
Kama Antonio Conte atakutwa na hatia huenda akakutana na kifungo cha miezi sita cha kutojihusisha na soka, Conte alituhumiwa kujihusisha na upangaji wa matokeo msimu wa 2010-2011 wakati akiwa kocha wa klabu ya Siena ya Italia.
Previous
Next Post »