Mbio za ubingwa wa ligi kuu ya England kwa timu ya Leicester zimepunguzwa kasi baada ya leo kulazimishwa sare na West Ham United.
Katika mechezo ulipigwa leo dimba la King Power Leiceister ikiwa nyumbani, dakika 90 zimemalizika kwa sare ya mabao 2-2 na kufanya miamba hiyo ambayo imo katika nafasi sita za juu kugawana point 1 kila moja.
Leiceister ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Jamie Vardy katika dakika ya 18, na hadi kipindi cha kwanza kinakamilika, matokeo yalikuwa ni 1-0.
West Ham walifanikiwa kuchomoa dakika ya 84 kwa njia ya penati iliyofungwa na Andy Carroll kabla ya Aaron Cresswell kupiga la pili dakika ya 86 ambapo Leicester walikuwa pungufu uwanjani.
Leicester hawakukata tama na kupambana ambapo walifanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika za nyongeza, ikiwa ni sekunde chache kabla mpira haujamalizika na kufa matokeo yawe ni sare ya 2-2.
Mbali na kuambulia pointi moja, Leicester imepata pigo baada ya mshambuliaji wake tegemeo na mfungaji wa bao la kwanza Jamie Vardy kuambulia kadi nyekundu dakika ya 56 baada ya kupata kadi mbili za manjano, na hivyo kukosa mchezo unaofuata.
Kwa matokeo hayo Leicester imefikisha point 73 kwa michezo 34 ikiwa mbele ya Tottenham Hotspur yenye point 65 na michezo 33.
Kesho Jumatatu, Tottenham itakuwa ugenini dhidi ya Stoke City.
Kesho Jumatatu, Tottenham itakuwa ugenini dhidi ya Stoke City.
Katika mchezo mwingine Liverpool ikiwa ugenini imefanikiwa kuicharaza AFC Bounermouth mabao 2-1 yakifungwa na Firmonho dakika ya 41 na Sturridge dakika ya 45, na hivyo kufanikiwa kufikisha point 51 katika nafasi ya 8.
Sign up here with your email
