KENYA YAITAKA ICC KUIKABIDHI FAILI ZA WASHIKIWA. - Rhevan Media

KENYA YAITAKA ICC KUIKABIDHI FAILI ZA WASHIKIWA.

Image captionMwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai
Kenya sasa inataka faili za kesi zinazowakabili wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia ushahidi wa mashahidi wa ICC kushtakiwa nchini humo.
Mwanasheria mkuu Profesa Githu Muigai amesema kuwa Kenya ina mahakama zilizo na uwezo za kushtaki kesi ndogo kufuatia kuanguka kwa kesi kuu iliowahusisha wakenya sita maarufu kama Ocampo 6.
Mwanasheria huyo pia ameshtumu idara ya mashtaka katika mahakama ya ICC kwa kushindwa kushirikiana na Kenya kuhusu ombi la awali lililowasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka Moreno Ocampo kuikabidhi Kenya faili zote za washukiwa.
Image captionMahakama ya ICC
Amesema kuwa Kenya ina haki ya kushirikiana na mahakama hiyo au la iwapo ICC itafeli kuikabidhi Kenya faili hizo.
Ameongezea kuwa mpango wa Kenya kujiondoa katika mahakama hiyo utaangaziwa na Umoja wa Afrika AU na kwamba Kenya kama taifa haijaanza harakati za kujiondoa.
Previous
Next Post »