KARIBUNI MIILI 350 YA WAISLAMU IMEPATIKANA IKIWA IMEZIKWA KWA SIRI , KASKAZINI MWA NIGERIA. - Rhevan Media

KARIBUNI MIILI 350 YA WAISLAMU IMEPATIKANA IKIWA IMEZIKWA KWA SIRI , KASKAZINI MWA NIGERIA.


Karibu miili 350 ya Waislamu imepatikana ikiwa imezikwa kwa siri katika kaburi la umati kaskazini mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kano, Muhammad Namadi Musa, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Wafuasi wa Dini Mbalimbali amesema kugunduliwa kaburi hili la umati ni ushahidi wa wazi kuwa mamia ya Waislamu waliuawa Desemba mwaka jana wakati jeshi la Nigeria lilipowashambulia Waislamu wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria katika jimbo la Zaria. 

Katika tukio hilo, jeshi la Nigeria liliwafyatulia risasa wafuasi wa harakati hiyo inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye sasa anashikiliwa na jeshi la nchi hiyo akiwa na majeraha na risasi mwilini.

Siku ya Jumatatu mwanaharakati mmoja maarufu wa nchini Uingereza alikosoa vikali ukimya wa jamii ya kimataifa juu ya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu nchini Nigeria.


Masoud Shajareh mkuu wa Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu (IHRC) yenye makao yake London amesema ni miezi kadhaa sasa imepita tangu kujiri mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu nchini Nigeria ambapo hadi sasa ukatili huo haujachunguzwa.
Previous
Next Post »