IDADI YA WATUMISHI HEWA SHINYANGA YAONGEZEKA MARA DUFU. - Rhevan Media

IDADI YA WATUMISHI HEWA SHINYANGA YAONGEZEKA MARA DUFU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema mpaka sasa idadi ya watumishi hewa mkoani shinyanga imetoka 0 hadi 226.
Rais ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa daraja la Kigamboni ambalo pia amependekeza kama Wizara ya Ujenzi itaridhia liitwe daraja la Nyerere.
Wakati akiendelea na hotuba yake Rais Magufuli alipata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam paul Makonda kwamba stendi ya Ubungo huingiza hasara ya milioni 42 kwa mwezi kutokana na mkataba aliosaini Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Wilson Kabwe ambapo Rais Magufuli akatangaza kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo.
Baada ya Rais kutangaza uamuzi huo akawataka viongozi watakao pata nafasi katika serikali yake kuhakikisha wanafanya kazi kwa maslahi ya watanzania wanyonge tofauti na hapo hatawavumilia.
''Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana wafanyakazi hewa 226 kutoka 'zero' hivyo ni lazima tuwajibike kwa watanzania wanyonge''-Amesema Rais Magufuli.
Aidha wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna mtumishi hewa hata mmoja jambo ambalo Rais aliunda tume iliyobaini watumishi 45 kwa awali ndipo Rais akatangaza kutengua uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na wasaidizi wake.
Previous
Next Post »