HUU NDIO UTAFITI WA UJANGILI WA MENO YA TEMBO. - Rhevan Media

HUU NDIO UTAFITI WA UJANGILI WA MENO YA TEMBO.



Ripoti ya utafiti kuhusu ujangili wa meno ya tembo imebaini kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi mbili za Afrika ambazo idadi kubwa ya tembo wanauawa. Utafiti huo umebaini kuwa asilimia 85 ya meno ya tembo yanayokamatwa asili yake ni mbuga za Selous, Ruaha na Ruangwa, Tanzania. Kadhalika, utafiti huo umebaini kuwa nchi nyingine ambayo tembo wengi wanauawa ni Congo. Katika utafiti huo, Mwanabaiolojia wa Chuo Kikuu cha Washington, Samuel Wasser alitumia teknolojia ya vinasaba kujua asili ya meno ya tembo yanayokamatwa. “Kujua maeneo ambayo meno mengi yanatoka, kunasaidia kujua eneo lenyewe na kuwekeza nguvu kazi na sheria ili kumaliza mauaji ya tembo,” alisema Wasser. Katika utafiti huo, Wasser alitumia sampuli za vinasaba kama kinyesi cha tembo, tishu na nywele ambavyo alivikusanya kutoka katika nchi zote Afrika. Baadaye alioanisha vinasaba hivyo na meno yaliyokuwa yakikamatwa. Maabara iliyofanya utafiti huu ilipokea meno ya tembo yanayokamatwa na shirika la kimataifa la uchunguzi (jina linahifadhiwa) kisha baadaye yalipimwa ili kujua asili yake. Kwa mfano, Julai 2006, kilo 2,500 za meno ya tembo yenye vinasaba vya Tanzania, yalikamatwa katika Jimbo la Kaohsiung, Taiwan. Lakini kiasi kikubwa cha meno ya tembo kutoka Tanzania kilikuwa ni kilo 6,034 zilizokamatwa Desemba 2012, Port Klang, Malaysia
Previous
Next Post »