HII NDIYO CHINA WAPANIA KUJENGA VIWANJA 60,000 VYA KANDANDA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 6 - Rhevan Media

HII NDIYO CHINA WAPANIA KUJENGA VIWANJA 60,000 VYA KANDANDA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 6

Image copyrightBBC CHINESE
Image captionViwanja elfu 60 vitakarabatiwa na vingine kujengwa upya.
China inapania kujenga viwanja 60,000 vya Kandanda katika kipindi cha miaka 6 ijayo.
Image captionUwanja wa taifa wa Beijing
Hayo ni baadhi ya mapendekezo katika ruwaza ya kandanda ya China ya 2050 ya kuifanya nchi hiyo iwe kati ya mataifa makuu duniani katika kandanda.
Ripoti moja ya serikali imeelezea mipango ya kuimarisha idadi ya wachezaji na watoto wanaosakata dimba kutimia watoto milioni 50.
Image copyrightXinhua News Agency
Image captionChina inalenga kuwa na wachezaji milioni 50 katika miaka 30 ijayo
Viwanja elfu 60 vitakarabatiwa na vingine kujengwa upya.
Kulingana na ruwaza hiyo China itakuwa na vilabu vyenye hadhi ya kimataifa kufikia mwaka wa 2050.
Image copyrightGetty
Image captionRais Xi Jinping amenukuliwa akisema kuwa angeli furahishwa mno iwapo timu ya taifa ya China ingelifuzu tena kwa kombe la dunia
Rais Xi Jinping amenukuliwa akisema kuwa angeli furahishwa mno iwapo timu ya taifa ya China ingelifuzu tena kwa kombe la dunia la kandanda na hata kushinda kombe la dunia.
Aidha rais Jinping pia anaitaka kombe la dunia la kandanda liandaliwa nchini mwake.
Previous
Next Post »