DENI LA TAIFA LAONGEZEKA MARADUFU KAMBI RASMI YA UPINZANI WASHTUKA. - Rhevan Media

DENI LA TAIFA LAONGEZEKA MARADUFU KAMBI RASMI YA UPINZANI WASHTUKA.



Deni la taifa limeongezeka maradufu, hali ambayo imeifanya kambi Rasmi ya Upinzani kushtuka na kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum.Ongezeko hilo, kwa mujibu wa kambi ya upinzani, deni hilo limeongezeka kwa kiasi hivyo, kutoka mwaka 2010 hadi mwaka jana.Akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2011/12 hadi 2015/16 na mwelekeo wa Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2015/16 hadi 2020/21, Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde, alisema hali ya deni la taifa inatisha na Bunge linapaswa kushituka.Silinde alisema nchi itafilisika kama Ugiriki ikiwa Bunge halitachukua hatua madhubuti za kuisimamia serikali.Alisema deni la taifa limekuwa na kufikia dola za Marekani bilioni 19.141 (Sh. trilioni 41.536). Alisema deni liliongezeka maradufu mwaka jana, baada ya serikali kukopa dola bilioni 3.846 (Sh. trilioni 8.347)."Mwishoni mwa Juni, 2010, jumla ya deni la Tanzania lilifikia dola bilioni 9.9 (Sh. trilioni 13.6) kulingana na thamani ya dola kipindi hicho). Miaka mitano baadaye deni limefikia Sh. trilioni 41.5, lazima Bunge tushituke," alisema Silinde.
Previous
Next Post »