Waziri
wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage akizungumza na kukaribisha
Ujumbu wa Wataalamu kutoka nchini Japani katika mradi wa ushauri wa
kuwekeza katika Rasirimali watu na vitendeakazi ili kuzalisha kwa tija
na ubora wa bidhaa kupitia mradi wa KAIZEN ili kuwekeza zaidi kwa namna
unavyozalisha na kufanya kazi kwa tija, wakati wataalamu hao
walipokutana na Waziri huyo wataalamu mbalimbali wa Wizara ya Viwanda na
Biashara katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
wizara hiyo mwishoni mwa wiki.
Waziri
Mwijage amesema wataalamu hao wanashauri mambo mengi katika uzalishaji
wa bidhaa na kilimo kama vile kuwapa uelewa zaidi wataalamu na
wajasiriamali wenyewe ili kuwekeza katika viwanda na kilimo kwa tija na
ubora ili kufikia malengo ya kuwafanya watu kuwekeza kwa tija na
ufanisi, Ukielewa namna nzuri ya uwekezaji wenye tija na ubora utaweza
kufaidika na uwekezaji wako bila kutumia nguvu na gharama kubwa sana
bila mafanikio.
Katika
picha kulia ni Profesa Tetsushi Sonobe Makamu wa rais wa Shirika la
GRIPS la Japan na katikati ni Profesa Toshio Nagase Mwakilishi wa
shirika la JICA nchini Tanzania.
Profesa
Toshio Nagase Mwakilishi wa shirika la JICA nchini Tanzania akitoa
utambulisho wa ujumbe aliofuatana nao katika mkutano huo uliofanyika
katika Wizara ya Viwanda na Biashara mwishoni mwa wiki.
Sign up here with your email