Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na watendaji kutoka Shirika la
Maendeleo la Ufaransa (AFD), Mwakilishi wa Shirika hilo nchini, Emmanuel Baudran (katikati) na
kushoto ni Dennis Munuve kutoka Shirika hilo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) akiwa katika kikao na
watendaji kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.
Na Teresia Mhagama,
Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) limesema kuwa limeshatoa jumla
ya Euro milioni 321 kuanzia mwaka 2009 mpaka sasa ambazo ni sawa na
wastani wa Euro milioni 50 kwa mwaka kwa ajili ya shughuli za maendeleo
nchini na kwamba mpango wake ni kuongeza kiwango hicho ifikapo
mwakani.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania,
Emmanuel Baudran wakati alipofika Wizara ya Nishati na Madini ili
kuzungumza masuala mbalimbali na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo pamoja na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na
Madini na Taasisi zake.
Baudran alieleza kuwa fedha hizo ambazo zimetolewa kupitia mkopo
wenye masharti nafuu zimeelekezwa katika Sekta za Maji, Nishati na
Miundombinu ya usafirishaji.
BONYEZA KITUFE CHA HOME KUTAZAMA BLOGU HII.
BONYEZA KITUFE CHA HOME KUTAZAMA BLOGU HII.
Sign up here with your email