TANZANIA KUJITEGEMEA KWA ASILIMIA 80 WAZIRI KASSIM ABAINISHA. - Rhevan Media

TANZANIA KUJITEGEMEA KWA ASILIMIA 80 WAZIRI KASSIM ABAINISHA.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaweza kujitegemea kwa zaidi ya asilimia 80 katika bajeti yake kutokana na vyanzo vyake vya ndani. Amesema Tanzania ina rasilimali nyingi na vyanzo vingi vya mapato, asema mapambano dhidi ya ufisadi ni endelevu Amesema hili linawezekana, ndio maana tumeamua kubanana,” alieleza Waziri Mkuu. Alisema ndio maana wameamua kupambana na ufisadi na ukwepaji kodi kwa nia ya kuhakikisha wanapata fedha za kuwatumikia Watanzania kwa fedha za ndani kupitia mapato yake. Alisema hata uamuzi wa kupitisha fedha zote katika Mfuko Mkuu wa Serikali ulikuwa na nia ya kutambua mapato yake yote ili fedha hizo zikasaidie kuleta maendeleo ikiwamo kuisimamia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kubana mianya yote ya ukwepaji kodi. Alisema hali hiyo imesaidia kwani mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni 1.3 Desemba mwaka jana, Sh bilioni 1.5 Januari mwaka huu na mwezi uliopita, alisema ana hakika zitavuka zaidi. Alisema kutokana na hali hiyo, serikali ndio maana inagharimia mambo yake mengi likiwamo suala la elimu bure, na kwamba licha ya kuwapo kwa changamoto mbalimbali, watahakikisha Watanzania wanapata huduma mbalimbali zilizoboreshwa.
Previous
Next Post »