
Rais Dk. John Magufuli amesema amejitolea kuwa sadaka kwa Tanzania katika vita dhidi ya mafisadi na kwamba akishindwa kufanya hivyo, hakuna sababu ya yeye kuitwa rais.
Pia amesema wote waliotumbuliwa majipu watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Akizungumza jana katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika sehemu ya barabara ya Sakina hadi Tengeru yenye urefu wa kilomita 14.1, itakayokuwa na njia nne, alisema ataendelea kutumbua majipu kwa kuwa wanaonufaika na kudidimiza uchumi wa nchi ni wachache.
“Tumeanza kuchukua hatua ndogo ndogo, tunatumbua majipu. Mpaka sasa waliotumbuliwa si wengi kiasi hicho, hawajafika hata 2,000. Juzi juzi nimesikia baadhi ya watu wameanza kuwatetea wanaotumbuliwa, nasema hao wanaowatetea washindwe na walegee,” alisema.
Sign up here with your email
