KAMPUNI ya Samsung nchini Tanzania imezindua simu mpya ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City jijini Dar es Salam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja mafunzo wa bidhaa za Samsung, Julius
Giabe mara baada ya uzinduzi alisema simu ya Samsung Galaxy S7 ni toleo
jipya ambalo kwa sasa inapatikana madukani kote nchini.
Amewaomba
watanzania wajitokeze kununu simu hiyo yenye ubora wa hali ya juu kwani
imeboreshwa zaidi kulingana na tekinolojia ya sasa.
Alisema
Julius Samsung Galaxy S7 imeboreshwa zaidi kwenye upande wa Camera
kwani ina Mega Pixel 12 zilizoboreshwa zaidi kiasi ambacho unaweza
kupata picha au Video nzuri zaidi.
Kioo chake kizuri cha kuvutia na inazuia vumbi na Maji kwa muda wa dakika 30 ndani y maji.
Julius
alisema, Samsung Galaxy S7 inakaa na chaji kwa muda mrefu sana na hata
ikiisha chaji inauwezo wa kuichaji bila kuchomeka kwenye Umeme(Wireless
charging).
Julius
alimaliza kwa kuwaomba watanzania tusikose kumiliki simu ya Samsung
Galaxy S7 ukakosa mambo mazuri katika teknolojia hii ya kisasa ambayo
Dunia yote iko Kiganjani mwako.
Kwa
wakazi wa Dar es Salaam tutembelee Mlimani City ambapo promosheni ya
Samsung Galaxy S7 inaendelea,upate kwa undani ubora wa simu hiyo.“Kuwa wa kwanza kumiliki simu ya Samsung Galaxy S7”.
Balozi
wa Samsung Tanzania,Aisha Saki(katikati) akiwaelezea jambo wateja
waliotembelea uzinduzi wa simu ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City jijini
Dar es Salaam.Kulia ni mabalozi wenzake.
Balozi
wa Samsung Tanzania,Rhoda Iddy(kulia) akimkabidhi mteja simu ya Samsung
Galaxy S7 baada ya kuinunua mara baada ya uzinduzi wa simu hiyo
uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Sign up here with your email