DONARD TRUMP ATISHIA KIJITOA KWENYE CHAMA. - Rhevan Media

DONARD TRUMP ATISHIA KIJITOA KWENYE CHAMA.


DONALD TRUMP AONGELEA DINI YA KIISLAM. - Rhevan Media


Licha ya Donald Trump kuongoza kwenye kura za maoni kupitia Chama cha Republican, ni dhahiri viongozi wake hawamtaki kwa kumtamkia wazi kwamba hafai.
Baada ya kugundua haungwi mkono, Trump alitishia kujitoa kwenye chama ili asimame kama mgombea binafsi endapo atafanyiwa mizengwe. Hali hiyo iliwapa kiwewe na wasiwasi viongozi wa Chama cha Republican.
Pia, alitangaza kwamba atamuunga mkono mgombea ambaye atateuliwa na chama hicho, huku akisisitiza kuwa bila shaka mgombea huyo atakuwa ni yeye (Trump).
Miongoni mwa vigogo hao waliopambana kufa na kupona ili kuhakikisha Trump hapati nafasi ya kuteuliwa kugombea nafasi ya urais ni mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2012, Mitt Romney.
Previous
Next Post »