SAKATA LA ESTER BULAYA MBUNGE WA CHADEMA. - Rhevan Media

SAKATA LA ESTER BULAYA MBUNGE WA CHADEMA.





Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema), alikamatwa juzi usiku akiwa hotelini jijini hapa na kusafirishwa jana kama mhalifu kwenda Dar es Salaam, kwa amri ya Bunge.
Bulaya alikamatwa wakati vikao vya Kamati Kuu na Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) vikiendelea. 
Baada ya kukamatwa, Bulaya aliwekwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi Mwanza, kabla ya jana saa 4.30 asubuhi kupakiwa kwenye gari la polisi chini ya ulinzi mkali hadi uwanja wa ndege wa Mwanza, kwa ajili ya kupelekwa Dar kujibu tuhuma zinazomkabili.Bulaya alisindikizwa na magari kadhaa ya polisi likiwamo Toyota Landcruiser T 387 DCP ya Ofisa Upelelezi wa Mkoa, PT 3643 na T 916 ASC.Kwa mujibu wa habari kutoka kwa watu wa karibu na Mbunge huyo, Bulaya alikamatwa kutokana na amri ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa madai kwamba hakuhudhuria kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge iliyomuita kumuhoji.
Previous
Next Post »