MTUHUMIWA WA RUSHWA KESI YA ESROW YUPO HURU. - Rhevan Media

MTUHUMIWA WA RUSHWA KESI YA ESROW YUPO HURU.





Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemfutia mashitaka ya kupokea rushwa ya Sh. milioni 161.7 za Tegeta Escrow, Mkurugenzi wa Fedha Benki Kuu Tanzania (BoT), Julius Angelo (49), baada ya upande wa Jamhuri kusema hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Uamuzi huo ulielezwa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, baada ya upande wa mashitaka kwa kutumia kifungu cha 98 (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kuiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo.
Kwa upande wake, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Max Ally, alieleza kuwa, kesi hiyo ilipangwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri jana.Hakimu Shahidi alisema kwa kuwa upande wa Jamhuri umeona hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo, mahakama inaifuta na kumwachia huru mshtakiwa chini ya kifungu hicho.Januari 16, 2015, kigogo huyo wa BoT, alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, akikabiliwa na mashtaka ya kupokea rushwa.
Ilidaiwa kuwa, Februari 6, 2014 katika benki ya Mkombozi, jijini Dar es Salaam, alipokea Sh. milioni 161.7 kupitia akaunti namba 00120102646201.
Previous
Next Post »