Mwana dada Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ni kama sasa amedhamiria kutoka kimataifa zaidi kwa lengo la kujiongezea mashabiki wa ndani na nje ya nchi kwa kuanza maandalizi ya kumshirikisha msanii wa Marekani,Nicki Minaj.
Shilole alisema jana kuwa ili kujiimarisha kwenye kazi hiyo ya muziki hana budi kushirikiana na wasanii nyota wa nje ili afikie mafanikio.
”Hapa nilipo ninajiandaa kwenda kufanya kolabo na Nicki Minaj baadhi ya watu wamekuwa wakishangaa baada ya kusikia habari hiyo,ukweli uko hivyo na nilishawahi kuweka wazi mipango yangu ya kushirikiana na nyota huyo,” alisema Shishi.
Hata hivyo,alitaja changamoto ya kutojua Kiingereza inakwamisha baadhi ya mipango yake ya na sasa ameamua kurudi shule ili kujifunza lugha hiyo na hatimaye kukamilisha mikakati yake.
Alisema kuwa penye nia pana njia na kwamba anaamini mipango yake itakwenda sawa na atatimiza kile alichokusudia kukifanya kwa manufaa yake.
Sign up here with your email
