Wimbo wake mpya ‘Bado’ ndio unasumbua sasa hivi kwenye stations mbali mbali za Radio na TV, taarifa nzuri inabidi uifahamu kwamba mkali huyu amekwisha kamilisha album na itaachiwa mwezi wa tatu mwishoni.
Akizungumza , Harmonize amesema yeye kila siku huwa anafikiria kuandika na kufanya ‘ngoma’ mpya.
“Nashukuru mungu huwa natumia muda mwingi kuandaa kazi mpya, nmeshakamilisha nyimbo za kukidhi album, inshaalah mwezi wa tatu mwishoni ‘menejimenti’ yangu itakaa ili kuweza kuiachia” amesema.
Katika ‘line’ nyingine Mkali huyo ameweka wazi changamoto walizozipata wakati wa kufanya video ya Bado, ikiwa ni pamoja na kuharibu Piki Piki iliyotumika hali iliyowapelekea kulipa zaidi ya Dolla 4000.
Sign up here with your email
