
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amepiga marufuku utoaji wa vibali vya malori ya mizigo na magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia katika barabara zote zinazosimamiwa na Manispaa za jiji la Dar es Salaam.
Barabara hizo ni zile zilizojengwa kwa kiwango cha lami na hatua hiyo inatokana na barabara hizo kuharibika kwa kipindi kifupi kutokana uzito jambo linaloisababishia Serikali hasara.
“Kuanzia leo katika mkoa wangu ni marufuku kutoa vibali vya magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia kwenye barabara zetu, tunataka barabara zidumu, watakaokaidi watachukuliwa hatua,” alisisitiza Sadiki.Sadiki aliziagiza manispaa za jiji hilo kuweka alama za barabarani zinazoonesha zuio kwa magari yote yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kupita kwenye barabara hizo ili wamiliki na madereva watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua kali za kisheria.Alikuwa akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam kwenye kikao cha kwanza kwa mwaka 2016. Alisema manispaa za jiji hilo zinatenga fedha nyingi kujenga barabara mpya na kufanya matengenezo ya zilizopo lakini nyingi zinaharibiwa na malori ya mizigo.
Sign up here with your email
