JENGO JIPYA LAZINDULIWA MUHIMBILI. - Rhevan Media

JENGO JIPYA LAZINDULIWA MUHIMBILI.



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamisi Kigwangalla amezindua chumba kipya cha kulaza wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika jengo la Mwaisela, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam.Uzinduzi huo wa huduma bora, umetajwa kuwa ni njia ya kuelekea kuondokana na kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Dk Kigwangallah alisema ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa, serikali itaondoa huduma ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu na ndiyo maana inaendelea kuboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo ya taifa.Alisema huduma hiyo itatolewa kwa gharama nafuu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alisema wizara inaangalia vizuri jinsi ya kuondoa utaratibu huo wa kupeleka wagonjwa nje. “Sasa muanze kujipanga hapa Muhimbili.Endapo kutakuwepo na mgonjwa anayetaka kwenda nje idara husika ndiyo itampeleka baada ya kujiridhisha wao wameshindwa kumtibu. Hapa kazi tu haya ndiyo mabadiliko ya kweli ya serikali ya awamu ya tano tunayoyaleta. “
Previous
Next Post »