
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema ndani ya CCM kuna watu majipu ambao wameficha makucha ili wasijulikane uovu wao.Samia alisema hayo juzi alipozungumza na viongozi wa CCM kutoka wilaya zote za mkoa wa Tanga na wabunge wa mkoa huo katika ukumbi wa CCM jijini Tanga.
Alisema ndani ya chama cha CCM kuna watu ambao ni watendaji wa serikali ambao hawarekebishiki kwa kuwa wamejificha ndani ya chama ili kuficha mambo yao.Alisema kuna watu wamo ndani ya CCM wanafanya biashara lakini hawalipi kodi ya mapato serikalini. Samia alikemea tabia hiyo na kuagiza viongozi wa CCM kuwabana watu hao na kuziba mianya ya kukwepa kodi ili kuongeza mapato ya serikali.Pia alisema ndani ya chama hicho kuna wanafiki kama mchwa wanafukuta ndani kwa kuharibu chama na kusababisha watu wagombane. Aliwataka watu hao wondoke mapema ndani ya chama ili kuendelee kuwa salama na kuongoza nchi.
Sign up here with your email
