BIFU LA PAUL MAKONDA NA SAID KUBENEA LAKUWA. - Rhevan Media

BIFU LA PAUL MAKONDA NA SAID KUBENEA LAKUWA.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Saed Kubenea, ana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma za kutoa lugha ya matusi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri.Hakimu Simba alisema ushahidi uliotolewa unaonyesha maswali dhidi ya mshtakiwa na kwamba anatakiwa kupanda kizimbani kujitetea.Alisema ushahidi wa upande wa utetezi utaanza kusikilizwa Machi 7, mwaka huu.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alisema upande wake unatarajia kuita mashahidi wanne akiwamo mshtakiwa.Hakimu Simba alisema dhamana ya mshtakiwa inaendelea na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa ushahidi wa utetezi Machi 7, mwaka huu.


Previous
Next Post »