
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametangaza kuwa serikali imewalipa makandarasi Sh bilioni 400, ikiwa ni malimbikizo ya madeni yao. Amewaagiza makandarasi wote wa ujenzi wa barabara, waliokuwa wamesitisha kazi zao kutokana na madai yao, kurejea kazini mara moja.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imewalipa makandarasi hao Sh bilioni 400 kati ya deni lao la zaidi ya Sh trilioni moja ; na kwamba mpaka kufikia Juni mwaka huu, makandarasi wote watakuwa wamelipwa fedha zao.
Waziri Mbarawa aliyasema hayo juzi wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro, alipotembelea wilaya ya Mvomero kukagua uharibifu wa miundombinu ya barabara na daraja la Diwale lililopo eneo la Mvomero – Turiani.
Sign up here with your email