Kwako Mh raisi John Pombe Magufuli.
Mh raisi kwanza nikupongeze kwa moyo wa dhati kwa kuonesha kukerwa wizi,uzembe na ukwapuaji wa mali za umma,ukweli taifa letu lilikuwa linakwenda kuzimu,tulianza kubadili mabaya kuwa mazuri,na mazuri yakageuzwa kuwa mabaya,wapenda haki walianza kugeuzwa kuwa maadui ndani ya jamii yetu,kwa hili nakupongeza,endelea hivi hivi.
Mh raisi kwanza nikupongeze kwa moyo wa dhati kwa kuonesha kukerwa wizi,uzembe na ukwapuaji wa mali za umma,ukweli taifa letu lilikuwa linakwenda kuzimu,tulianza kubadili mabaya kuwa mazuri,na mazuri yakageuzwa kuwa mabaya,wapenda haki walianza kugeuzwa kuwa maadui ndani ya jamii yetu,kwa hili nakupongeza,endelea hivi hivi.
Utumbuaji huu wa majipu kila siku naamini kama ungeachwa kwa miaka miwili,nchi hii ingekuwa imekwisha,watu walikuwa wanakwapua mali za umma bila haya,watu walikuwa na mali ambazo hazilingani na vipato vyao,shughuli za kijanja ndiyo zilikuwa zina heshima,ofisi za umma zilitaka kugeuzwa kuwa vijiwe vya kupiga deal la kuifilisi nchi,hongera sana Mh raisi kwa ujasiri huu,waizi walikuwa wanasifiwa,huku waadilifu wakibezwa na kuitwa washamba.tumbua majipu yote usiache hata moja,kila jipu lazima litumbuliwe
Mh raisi pamoja na kuonesha nia ya dhati ya kupambana na wizi wa mali za umma,naona bado kuna eneo moja linahitaji ulifanyie kazi,vinginevyo utamaliza miaka mitano bila watanzania kuona matokeo kwa moja ya juhudi zako za kutumbua majipu ambayo kwa kiasi Fulani yamekupa sifa kwa wanaanchi,hii ni kutokana na taifa letu kutafunwa na mdudu rushwa kwa kipindi kirefu.
Mh Raisi,naona si wananachi wa kawaiada tu,badi hata wasaidizi wako wa karibu(mawaziri) itakuwa hawajui unataka kujenga nchi ya namna gani,matokeo yake tunashuhudia viongozi wako wakiruka ruka huku na kule wengine wakidumbukia kwenye madibwi ya maji,wengine wanakwenda kufagia.
Mwalimu Nyerere wakati wa utawala wake pamoja na kushindwa kutimiza ndoto zake kwa asilimia 100,lakini alihakikisha wananchi wote na hasa wasaidizi wake wanajua dira,falsafa na itikadi ya nchi,mwalimu alihakikishi kila mtanzania anafahamu kuwa katika kila analolifanya kusudio lake kuu ni kujenga nchi ya ujamaa na kujitegemea,mwalimu alikuwa akiingia darasani,katika kila analofundisha lililenga kujenga nchi ya ujamaa na kujitegemea,mwandishi alijua kila anachoandika alijua kusudia lake ni kujenga nchi ya ujamaa na kujitegemea,mkulima anapolima alijua analima ili kuhakikisha Tanzania inaondokana na utegemezi.
Wamarekani wanajua fika,kila raia ana wajibu wa kujenga taifa kubwa na lenye nguvu duniani,wanajua lengo kuu la Marekani ni kubaki kuwa taifa kubwa la kibepari lenye nguvu,huko uchina napo raia wanajua kila wanachofanya ni kuhakikisha wanajenga taifa kubwa la kikomunisti litakaloutawala ulimwengu,waingereza hususani Ireland wanajua kazi ya kila raia wa Ireland ni kuhakikisha Lugha yao inautawala ulimwengu,wanakazi ya kuhakikisha ulimwengu mzima unazungumza lugha yao,wanataka kuhakikisha wanautawala ulimwengu kwa lugha yao na hilo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwakuifanya lugha yao kuwa bora ulimwenguni,leo ili mtu aonekane msomi,hana budi kuzungumza kwa ufasaha lugha ya kisiwa cha Ireland na kudharau yake.
Mh Magufuli,wewe unataka kujenga taifa la namna gani?falsafa yako ni ipi?dira yako ni ipi?itikadi yako ni ipi?je bado unataka kujenga taifa ya kijamaa?weka wazi maono ya dira yako Mh raisi.
Mh Raisi,sasa tunashuhudia wasaidizi wako wakirukaruka huku na huko,leo tunashuhudia mawaziri wako wanafagia kwenye maofisi huku kuna watu wameajiriwa kufanya usafi,tunashuhudia mawaziri wako wanawakamata wakwepa kodi na TAKUKURU ipo kimya,yenyewe haikamati ,tunashuhudia wakuu wako wa wilaya wanakwenda field na kuanza kutumbukia kwenye matope,wengine wanapanda bodoboda bila hata kuvaa helmet,hapa kuna shida Mh Raisi.
Moja ya dhana ama nguzo za utawala bora ni UWAJIBIKAJI,mh raisi nikuponeze kwa hili,ila nikukumbushe kuwa dhana hii imegawanyika katika maeneo makuu mawili yenye matawi matatu,na uwajaibikaji wa pamoja na uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja ama taasisi moja,sasa tunachokishuhudia sasa ni uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja(Individual Accountability).
Leo tunaona waziri mkuu anakwenda kamata wakwepa kodi pale bandarini,ni jambo zuri sana kwa mtazamo wa uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja,shaka iliyopo hapa,kwa nini tangu umeingia madarakani,Takukuru hatujawahi kusikia imekamata wakwepa kodi na wala rushwa?kwa nini waziri mkuu ama waziri akakamate wakwepa kodi Bandarini,Aiport,MSD,ATCL,Takukuru wapo wapi?kwa nini hawakamati?ndiyo kusema Mh Waziri mkuu asipotoka ofisini,wanaopitisha makontena kwa njia za panya hawatakamatwa?
Je Mh waziri mkuu asingekwenda ATCL hizo milioni 700 za tiketi zisingejulikana?kwa nini TAKUKURU hawakamati?Mh raisi jenga dhana ya uwajibikaji wa pamoja,taasisi zote,idara zote ziwajibike kwa pamoja,haiwezekani ukaendesha serikali ambayo taasisi na idara zote zikawa zimelala,hazichukui hatua yeyote,zinamsubiri waziri mkuu aende,Mh raisi vunja huu utamaduni wa uwajibikaji wa mtu mmoja ama taasisi moja,,jenga dhana ya utamaduni wa pamoja.
Yawezekana wasaidizi wako hawajui unataka kujenga nchi ya namna gani?ndiyo maana jana nimemuona waziri anafagia Muhimbili,mkuu wa wilaya anatumbukia kwenye mafuriko,wengine wanakwenda timiza wajibu kwa bodaboda bila kuvaa helmet,Mg raisi wasaidizi wako yawezekana wanachojua wao ni kutumbua majipu tu,ila hawajui dira na maono yako,siku majipu yakiisha watafanya nini?sema itikadi,falsafa na dira yako mh Raisi.
Mh raisi wazi itikadi yako,sekta binafsi hazijui lolote,uchumi wa ulimwengu sasa unaendeshwa kwa kutengeneza ubia kati ya sekta binafsi na serikali,mpaka sasa sekta binafsi nyingi hazijui zianzie wapi?wasaidizi wako serikalini wapo bize na sekta za umma,huwezi kujenga uchumi bila kuzijengea uwezo sekta binafsi na kuziingiza kwenye uendeshwaji wa uchumi wan chi,huwezi jenga nchi kwa kuegemea upande mmoja wa sekta za umma na kuzipiga teke sekta binafsi,huwezi jenga nchi kbinafsi ni dhaifu,mwaka 2009 serikali iliamua kuja na sera ya mabadiliko ya uendeshwaji wa uchumi kwa kutumia dhana ya PPP,si wewe raisi wala wasaidizi wako wanasikika kutoa elimu ya namna ya kuendesha nchi kwa dhana hii ya ubia.
Weka wazi msimamo wako kuhusu diplomasia ya uchumi,kusema eti umezuia safari za nje,haitasaidia kitu,Economic Diplomacy,ndiyo inaipaisha Marekani,China,Japan,India,Korea,Umoja wa Ulaya,tengeneza mkakati wa kiuchumi namna utakavyoimarisha uchumi kwa dhana ya diplomasia ya uchumi,angalia fursa zipo wapi?teuwa mabalozi kimkakati,Mh raisi Political diplomacy haipo siku hizi,naamini akina Balozo Mahiga watakusaidia sana.
Mh raisi suala la Zanzibar,usilipuuze ,nadhani unafahamu na unajuma nafasi ya Zanzibar katika muungano wetu,usukubali kuruhusu damu zimwagike Zanzibar,litakuwa doa kubwa kwao,kaa na wasaidizi wako,wanadiplomasia muangalie namna ya kutanzua mgongano wa kisiasa visiwani Zanzibar,mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar haujaanza leo,uliaanza tangu uchaguzi mkuu wa kwanza mwaka 1963 uliowaweka madarakani ZPP,na ZNP,ulikuwa mkubwa sana baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964,ukaja paa mwaka 1972 baada ya kifo cha mzee Karume,ukapaa zaidi baada yam zee Jumbe kuondoshwa madarakani mwaka 1984 na ukapaizwa zaidi na zaidi na uchaguzi wa mwaka 1985 uliozaa kura za maruhani,ukapaa tena mwaka 1986,ukapaa tena mwaka 1995 ,kwama 2001 ndiyo ukapaa zaidi na zaidi baada ya mauaji ya baadhi ya wafuasi wa CUF.
Mh Raisi,kuanzia Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete wote walikutana na mkwamo wa kisiasa huko Zanzibar,tafakari walikwama wapi,kaa na wasaidizi wako ili wakusaidie kizalendo na wewe umalize mkwamo huu,Mh raisi nadhani utakiuwa unafanhamu mwalimu na mzee Karume walioasisi muungano huu nao walipita katika kipindi kigumu sana,hata alipokuja mzee Jumbe nae aliingia kwenye mvutano na mwalimu,si kitu kidogo kuona raisi wa Zanzibar anavuliwa madaraka,yawezekana mkwamo ulio mbele yako ni mdogo sana kuliko hata mikwamo aliyokutana wasaidizi wako,usilipuuze suala la Zanzibar!lifanyie kazi,
Mh raisi,tangaza dira,tangaza falsafa,tangaza itikadi ya Tanzania unayotaka kuijenga,ili vizazi na vizazi vikukumbuke,ni ngumu sana kukumbukwa kwa utumbuaji wa majipu pekee pamoja na kwamba ni jambo zuri sana,sasa tangaza itikadi yako,majipu yakiisha wasaidizi wako watakuwa hawana la kufanya!.
Hakikisha inajulikana kuanzia kwenye majiji mpaka vijijini,Ikulu mpaka mitaani,Bungeni mpaka halmashaurini,kwenye mahoteli ya kitalii mpaka vilabuni,shule za awali mpaka vyuo vyuo vikuu,kwenye ndege mpaka kwenye bodaboda.,kwenye cabinet mpaka kwenye vikao vya serikali za mitaa,misibani mpaka kwenye sherehe,kila mtanzania ajue vision and mission yako!,wakati ni sasa usisubiri kesho,tangaza itikadi,falsafa na dira yako ili wabobezi wakupe mawazo,huwezi pata mawazo kupitia utumbuaji wa majipu peke yake.
Nakupongeza sana Mh raisi kwa kutumbua majipu,ziamshe taasisi,idara na sekta zote ziende na kasi yako,tupe falsafa,itikadi na dira yako mapema.
Wasalaam
Wasalaam
Sign up here with your email