Waziri wa mambo ya nje ya nchi, ushirikiano wa kimataifa na kikanda Africa Mashariki Balozi Dr. Augustine Mahiga ametoa kauli bungeni kuhususiana na sakata la wa kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kitanzania aliyepo nchini India ambapo amesema tayari waliofanya hivyo wamefikishwa mahakani.
Balozi Mahiga amesema jana walimuita balozi wa India aliyepo hapa nchini na kuzungumzia swala hilo na tayari serikali ya India kupitia waziri wake wa mambo ya nje wameomba radhi juu ya tukio hilo.
Akaongeza kuwa waliohusika kitendo kile cha kuwadhalilisha wanafunzi hao wamekwisha kamatwa na kufikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheria.
Mh Mahiga akasema kuwa serikali ya India pia imeaagiza kuwa wanafunzi wote wa Tanzani waliopo nchini humu kwa masomo wapatiwe ulinzi wakati wa kwenda na kurudi shuleani
Hata hivyo balozi Mahiga ametoa ufafanuzi wa kifo cha mwanafunzi na kusema kuwa aliyefariki hakuhusika na tukio la wanafunzi waliovamiwa bali aliyepata ajali ya pikipiki kwa kugonga nguzo ya taa na serikali inashughulikia taratibu za mazishi yake.
Sign up here with your email