Serikali imesema mashine ya CT-Scan iliyopelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ilichukuliwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia aliyetaka kujua kuhusu mashine hiyo kuchukuliwa Dodoma wakati Serikali inasema ilinunuliwa.
“Kwanza naitaka Serikali ieleze ukweli, ni kwa nini wanasema kuwa walinunua mashine ya CT-Scan wakati ilichukua mashine hiyo Hospitali ya Ben Mkapa ya Udom na je mnataka wananchi wa mkoa huu wafe?” alihoji Nkamia.

Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kununua mashine mpya ya CT-Scan kwa ajili ya MHN
Sign up here with your email