RAIS PIERE NKURUNZINZA LEO USO KWA USO NA BAN KIN MOON IKULU BURUNDI. - Rhevan Media

RAIS PIERE NKURUNZINZA LEO USO KWA USO NA BAN KIN MOON IKULU BURUNDI.



Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amepangiwa kukutana na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika juhudi za kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo. Bw Ban, aliyewasili nchini Burundi Jumatatu, atakutana na Bw Nkurunziza leo ikulu ya rais na baadaye wawili hao wanatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja. Baada ya kuwasili Jumatatu, Bw Ban alikutana na wawakilishi wakuu wa vyama vya siasa na kujadili amani na usalama. Mamia ya watu wameuawa na maelfu kutoroka makwao tangu kuanza kwa machafuko nchini humo mwezi Aprili mwaka jana baada ya Rais Nkurunziza kutangaza angewania urais kwa muhula wa tatu.
Previous
Next Post »