
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ameweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi kuongoza waangalizi wa uchaguzi miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Uganda unaofanyika leo Mwinyi ambaye Mei 8 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 91, ameteuliwa kuwa Kiongozi wa Waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Uganda na sasa amepiku rekodi iliyowekwa na Arthur Moody Awori, aliyeongoza timu ya waangalizi wa jumuiya hiyo waliosimamia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2015. Kipindi hiki akiwa nchini Uganda Rais Mstaafu Mwinyi anaendelea na ratiba yake ya kawaida ya kufanya mazoezi na kuswali swala zote kwa mujibu wa matakwa ya dini yake ya Kiislamu. Mwinyi ambaye Watanzania pia wanamfahamu kwa jina la utani la ‘Mzee Ruksa’ alizaliwa katika kijiji cha Kivure mkoani Pwani, mwaka 1925, pia ndiye mtu pekee hapa nchini ambaye amewahi kuwa Rais wa Zanzibar na kisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sign up here with your email