
Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli, amejikuta akibubujikwa na machozi wakati akizungumza na wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi, Mbuyu, jijini Dar es Salaam, alipokwenda kuwaaga. Mama Janeth alisoma katika shule hiyo tangu darasa la kwanza hadi la saba na baadae kuwa mwalimu kwa miaka 18 katika shule hiyo kabla ya mume wake, Rais John Magufuli, kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania. Akiwaaga walimu na wanafunzi shuleni hapo jana, Mama Janet alisema kwa sasa ana majukumu mengi zaidi ya kumsaidia Rais kwa kipindi kirefu, hivyo analazimika kuondoka. “Inaniwia vigumu kuwaaga kwani kwa sasa nitakuwa na majukumu zaidi katika kumsaidia mume wangu, Rais John Magufuli, katika shughuli zake za kuwatumikia Watanzania kwa kipindi kirefu. Nitazifikisha changamoto zenu na za walimu nchi nzima kwa shemeji yenu,” alisema.
Sign up here with your email