KURA YA KATIBA PEMBEKEZWA YAZUA KIZAAZAA. - Rhevan Media

KURA YA KATIBA PEMBEKEZWA YAZUA KIZAAZAA.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekanusha taarifa zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa mchakato wa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, uko mbioni kuanza. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima imebainisha kuwa yapo mambo kadhaa yanayohitajika kukamilika kabla ya kuanza rasmi kwa mchakato huo wa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa. Kailima alisema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar ambao uliahirishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ni moja ya mambo ambayo yanahitajika kukamilika ili kuiwezesha Zanzibar kushiriki katika mchakato huo.Aidha, taarifa hiyo pia imebainisha kuwa suala lingine ambalo halijakamilika ni kupatikana kwa wabunge watatu wa Viti Maalumu ambao kupatikana kwao ni lazima Jimbo la Kijitoupele Zanzibar likamilishe uchaguzi wake na kumpata mbunge.

Previous
Next Post »