
Anaitwa Abdalah Nyangalio,ni mkazi wa Temeke Dsm na mlemavu wa macho,katika hali yake hii ya ulemavu wa macho,Abdalah anamudu kufanya kazi ya ufundi wa cherehani,nilipokutana nae alinisimulia mengi kuhusu jinsi anavyoweza kupata vipimo vya mteja wake na kushona nguo zikiwemo suti bila kuona,Abdalah akikushika tu mkono hapo hapo anafahamu urefu na upana wako,kuanzia mikono,miguu na hata kiuno,Mungu ni mwingi wa rehema na waajabu!Abdalah ni fundi stadi kweli kweli,ulemavu wake wa macho haujamzuia kujiajiri kwa kuwa fundi cherehani!.Mungu amzidishie ubunifu zaidi na afya njema.
Sign up here with your email