
Tatizo la matumizi ya vipodozi vyenye viambata litangazwe kuwa janga la Taifa ERIKALI imetakiwa kutangaza tatizo la matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya sumu na pombe haramu za viroba kuwa janga la Taifa, kama ilivyo kwa dawa za kulevya nchini, kutokana na uingizwaji wa bidhaa hizo mkoani Mbeya kukithiri kwa kiwango kikubwa na kuathiri afya za watumiaji na kusababisha wengine kufariki kutokana na kutumia bidhaa feki. FikraPevu imejulishwa kuwa tatizo la kushamiri kwa bidhaa hizo katika mkoa wa huo umeongezeka mara dufu, licha ya serikali kupiga vita uuzwaji wa bidhaa feki ikiwemo vipodozi na pombe haramu ya viroba ambazo huingiwa nchini kinyemela katika mikoa iliyopo pembezoni mwa nchi jirani zinazozunguka mikoa hiyo nchini. Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wametoa kauli hiyo, wakati wakishiriki zoezi la kuteketeza vipodozi vyenye viambata vya sumu na pombe haramu za viroba ambalo limefanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa,Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA) Nyanda za Juu Kusini katika wilaya hiyo. Wananchi hao wamesema pombe hizo zimesababisha vijana wengi wilayani humo kupoteza maisha pamoja na kuathiriwa na vipodozi vyenye sumu vikiathiri vibaya ngozi za watumiaji na kulazimika kutoa kilio hicho kwa serikali ili iweze kutangaza bidhaa hizo kuwa janga la kitaifa ili kunusuru afya za watumiaji. Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka hiyo kutoka Nyanda za Juu Kusini, Yusto Walace, amesema mamlaka hiyo imeteketeza bidhaa mbalimbali zilizoingizwa nchini kinyume cha sheria na kuwa TFDA itaendelea kupambana na tatizo hilo ili kunusuru afya za watumiaji na kusema kuwa tatizo la kuzagaa kwa bidhaa hizo katika mkoa huo linaathiriwa na uwepo wa njia za panya ambazo hutumiwa na watu wasio waadilifu. Mkuu wa wilaya ya hiyo, Gulam Kifu, pamoja na kukiri kuwepo kwa bidhaa hizo kwa wingi wilayani Mbarali, ameitaka TFDA kushirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuongeza kasi ya mapambano dhida ya uingizwaji wa bidhaa hizo na kusema kilio cha vijana hao kutaka kutangazwa kwa janga hilo atakifikisha katika mamlaka husika. Naye, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, ameiambia FikraPevu kuwa jeshi lake lipo makini
Sign up here with your email