Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema kwa vile Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeshatangaza tarehe ya kurejewa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar yeye binafsi haoni umuhimu wa kurejewa kwa mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein .
Amesema mazungumzo hayo kwa sasa hayana tija yoyote kwa vile wananchi katika kipindi hiki wameanza kujiweka tayari wakijiandaa kupiga kura kufuatia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufuta matokeo ya uchaguzi tarehe 28 Oktoba mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Pemba akijiandaa kurejeakKisiwani Unguja baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu kisiwani Pemba kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo akiwa Mtendaji Mkuu wa Serikali Balozi Seif Ali Iddi alisema iwapo yapo malalamiko yoyote muhusika wake ana wajibu wa kwenda mahakamani kwa hivi sasa.
Balozi Seif alisema mazungumzo ya pamoja kati ya Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kuhusu kufutwa kwa uchaguzi mkuu yalifanyika kwa maombi ya Maalim Seif ambaye yeye binafsi ndiye aliyeamua kujiondoa kwenye maendeleo ya vikao vya mazungumzo hayo.
Sign up here with your email