
Agizo la Rais Dk. John Magufuli kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto la kutaka jengo lililokuwa likitumika kama ofisi ya kitengo cha afya ya uzazi na mtoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), lifanywe wodi ya wazazi ndani ya siku mbili, limewatoa jasho vigogo.Vigogo kutoka wizarani na wakurugenzi wa Muhimbili, jana walikuwa wakihaha kutekeleza agizo hilo.Tofauti na ambavyo ingetarajiwa kuwa uhamishaji samani na kupanga vitanda ungefanywa na watumishi wa ngazi za chini pekee, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mpoki Ulisubisya, akihamisha samani zilizokuwa kwenye ofisi hizo ili iweze kutumika kama wodi ndani ya saa 48, alizotoa Rais Magufuli. Mbali na Ulisubisya, wakurugenzi wengine wa wizara hiyo na wale waliokuwa wakitumia jengo hilo, kila mmoja alionekana akifanya kazi kuhakikisha vifaa vilivyokuwa kwenye ofisi hizo vinahamishwa na vitanda vinawekwa.“Hapa kazi tu si unaona tunatekeleza agizo la Rais? Tumekuja tangu asubuhi kutoa vitu vyote. Hapa hakuna mfanyakazi wa cheo chochote wote tunafanya kazi,” alisema mmoja wa wakurugenzi ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa madai si msemaji.
Sign up here with your email