FEDHA ZA AHADI YA RAIS ZAZUA TAFRANI. - Rhevan Media

FEDHA ZA AHADI YA RAIS ZAZUA TAFRANI.


Madiwani wa halimashauri ya wilaya ya moshi mkoani kilimanjaro wamekuwa na malumbano kuhusu matumizi ya fedha za ahadi ya rais ya kupeleka shilingi milioni hamsini kila kijiji  kwa ajili ya wanawake na vijana wakitaka fedha hizo zitumike kukamilisha miradi ya maendeleo ambayo haikutekelezwa mwaka jana.
Madiwani hao wamesema miradi mingi ya maendeleo  iliyokuwa inatekelezwa katika wilaya hiyo ikiwemo ya barabara hazijakamilika kutokana serikali kuchelewesha fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la madiwani halimashauri ya wilaya ya moshi mh.michael kilawila anasema ni vema serikali ikaelekeza fedha hizo katika halimashauri kuliko kuzipeleka katika vijiji kwa kuwa miradi ambayo haijakamilika ni mingi ikiwemo ujenzi wa maabar,barabara na maji.
 
Mkurugenzi wa halimashuri hiyo bw.fulgence mponji anakiri uwepo wa miradi mingi kutokamilika kutokana na ukosefu wa fedha na kwamba endapo  fedha hizo zitaletwa zitatumika kwa kazi iliyokusudiwa.
Previous
Next Post »