
Chama cha Wazalendo (ACT-Wazalendo) kimepongeza juhudi za Rais John Magufuli katika kupambana na rushwa na ufisadi na kumtaka pia kuangalia uwezekano wa kufuta posho za vikao katika mfumo wa utumishi wa umma, ikiwamo Bunge. Hayo yamebainishwa na kiongozi wa chama hicho, Kabwe Zitto alipokuwa akizungumzia mambo yaliyojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu, juzi.“Rais anatakiwa kugeukia suala la posho, afute posho za vikao kwa mfumo wa watumishi wa umma, ikiwamo Bunge na kuachana na matumizi ya magari ya anasa (mashangingi),” alisema Zitto. Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, alisema Serikali pia inatakiwa kuleta mabadiliko ya kimfumo, ikiwa ni pamoja na kubadili mikataba ya kinyonyaji ya rasilimali kama ya madini na mafuta na kuachana na kuagiza sukari nje na kufanya mabadiliko katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
Sign up here with your email